WAISLAM SINGIDA WAKUMBUSHWA KUFUATA MAFUNDISHO YA DINI YAO


Na Hemedi Munga

 Zikiwa zimepita siku tatu baada ya Waislamu duniani kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu kutoka mwaka 1444 mpaka 1445 H, huku Rais wa Zanzibari na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Hassan Mwinyi, kutangaza siku hiyo kuwa ni ya mapumziko kwa Zanzibar, waislamu katika maeneo tofauti Tanzania bara  wameiadhimisha siku hiyo kwa  matembezi mafupi.

Imamu Mkuu wa Msikiti wa Taqwa mjini Kiomboi, wilayani Iramba mkoani Singida, Sheikh Omari Hassan, amewakumbusha waumini hao kuyafuata yote yaliofundishwa na dini yao.

Shekih Hassan alitoa nasahaa hizo baada ya kuwaongoza waumini wa dini hiyo kuadhaimisha mwaka huo mpya kwa kufanya zafa katika baadhi ya mitaa ya mji huo.

" Hii ni sharehe hivyo waumini nendeni majumbani kwenu mkasherehekee kwa kumtii Mungu na Mtume wake," amesema.

Aidha, amemuomba Mungu aendelee  kuwapa afya njema katika mwaka huo mpya.

Pia, amemuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kupata hekima, busara na afya kutoka kwa Mungu kwa lengo la kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Imamu Msaidizi wa Msikiti huo, Sheikh Ponda Rukumbwe, amewakumbusha waumini hao kutoa zaka hususan mali ambazo zimepitiwa na mwaka.

Sheikh Rukumbwe amebainisha kuwa huo ndiio muda sahihi wa Waumini wanaomiliki mifugo, fedha  na nafaka baada ya kuvuna kutekeleza moja ya nguzo za dini hiyo.

Amesema mali zanazotolewa zaka ni pamoja na fedha, mbuzi, kondoo, ng"ombe na ngamia.

Aidha, amewahusia waumini hao kijitathimini kwa kina kwa lengo la kufanya mazuri yanayopendeza Mungu.


Imamu Mkuu wa Msikiti wa Taqwa mjini Kiomboi, wilayani Iramba mkoani Singida, Sheikh Omari Hassan (kushoto), akiwaongoza wiislamu katika matembezi ya kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu, mkoani humo. ( Picha na Hemedi Munga)


Waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu wakitembea katika mitaa mbalimbali ya mji wa kiomboi wilayani  Iramba mkoani singida kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu 1445 H.