Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro, Saidi Mrisho amewataka, walimu kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao wanapowafundisha mashuleni.
Mrisho amesema hayo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo, ikiwemo ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari.
Amesema ukuaji wa teknolojia na utandawazi ni jambo lisilokwepeka hivi sasa, hivyo walimu mtumike kuwafundisha watoto masuala muhimu bila kuacha kukemea vitendo vibaya kwa watoto, ikiwemo masuala ya ukatili kwa watoto mashuleni.
Mrisho amesema ifike wakati kila watumishi katika sekta ya elimu wawajibike kuhakikisha elimu inasonga mbele na kuleta matokeo chanya kwa Watanzania.
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walimu kushirikiana katika maelezi ya watoto ili kupunguza mmomonyoko wa maadili na tabia mbaya ambazo zitawaletea matatizo watoto ikiwa ni pamoja na matumizi ya bangi, ubakaji na ulawiti mashuleni
"Nimesikia baadhi ya malalamiko kutoka kwa walimu kutopata ushirikiano kutoka kwa maafisa wa Halmashauri pale wanapopeleka kero na kuanzia sasa nawataka watumishi wote kuwa kitu kimoja ili kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassani, kuleta maendeleo kwa Watanzania", amesema.
Kwa upande wa walimu wa shule hiyo, wamemshukuru Rais Samia, kwa mambo makubwa aliyofanya katika uongozi wake mwaka, ikiwemo kupatia vitendea kazi huu vishkwambi ambavyo vinawasaidia kwa mawasiliano kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali, wamelipwa fedha walizokuwa wanadai muda mrefu ambapo serikali imelipa kwa wakati.
Naye mwananchi wa Tarafa ya Kilombero, Subira Omari, amepongeza ziara hiyo kwa kuibua kero nyingi pamoja na kuunganisha mawasiliano baina ya wanachama na mashule, na ametoa mfano wa ujenzi wa shule za wazazi na huduma za maji, umeme na chakula kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCMWilaya Kilombero, Saidi Mrisho (katikati) akiwa na wajumbe wa kamati ya utekelezaji, wakati akikagua miradi ya maendeleo, wilayani humo. |