RAIS SAMIA AWAPANGIA VITUO VYA KAZI MABALOZI, WANNE WABADILISHIWA VITUO VYA KAZI


Rais Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi, wakiwemo mabalozi sita wateule aliowateua Mei 10, 2023.

Aidha Rais  amewabadilisha vituo vya kazi Mabalozi wanne.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa  Agosti 11,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus. Mabadiliko hayo ni ifuatavyo, 

Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi ni

i) Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman. Balozi Fatma anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Abasi Kilima ambaye amestaafu.

ii) Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada. Balozi Sokoine anachukua nafasi ya Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya ambaye mstaafu.

iii) Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria.

iv) Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Meja Jenerali Mwaisaka anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo ambaye amehamishiwa Cairo, Misri.

v). Gelasius Gaspar Byakanwa (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.  Byakanwa anachukua nafasi ya Balozi Jilly Maleko ambaye amestaafu.

vi). Habibu Awesi Mohamed (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Qatar. Mohamed anachukua nafasi ya

Balozi Mahadhi Juma Maalim ambaye amehamishiwa Kuala Lumpur, Malaysia.

vii). Imani Salum Njalikai (Balozi Mteule) kuwa  Balozi wa Tanzania nchini Algeria. Njalikai anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu ambaye amestaafu.

viii). Hassan Iddi Mwamweta (Balozi Mteule) kuwa  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani. Mwamweta anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Saleh Possi ambaye amehamishiwa Geneva, Uswisi.

ix) Dt. Mohamed Juma Abdallah (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.  Abdallah anachukua nafasi ya Balozi Ali Jabir Mwadini ambaye amehamishiwa Paris, Ufaransa.

Mabalozi waliohamishwa vituo

i) Balozi Ali Jabir Mwadini kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Balozi Mwadini anachukua nafasi ya Balozi Dk. William Shelukindo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

ii) Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri. Balozi Meja Jenerali Makanzo anachukua nafasi ya Balozi John Emmanuel Nchimbi ambaye anarejea nyumbani.

iii) Balozi Abdallah Saleh Possi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi. Balozi Possi anachukua nafasi ya Balozi Maimuna Tarishi ambaye amemaliza mkataba wake.

iv) Balozi Dk. John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda. Balozi Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Dk. Aziz P. Mlima ambaye amestaafu.

Mabalozi wateule wataapishwa Agosti 16, 2023 saa 05:00 asubuhi, Ikulu,

Chamwino jijini Dodoma.