UMOJA WA MACHIFU WAOONYA MACHIFU WANAOWACHONGANISHA NA SERIKALI NA BUNGE



MOJA wa Machifu Tanzania (UMT), umesema unaendeleaje kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na kuheshimu Muhimiri wa Bunge, hivyo haukubaliani na machifu wote wanaokwenda kinyume na serikali au mihili yake.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UMT, Tanzania Chifu Antonia Sangalali, alipozungumza na gazeti hili jana, huku akikanusha taarifa za Chifu wa Mkoa wa Mwanza, Kisendi Nsingwa aliyoitoa hivi karibuni jijini Dodoma, ya kutoridhishaa na maamuzi ya Bunge yanayochukuliwa dhidi ya Wabunge wanaokiuka sheria.

"Sisi Umoja wa Machifu Tanzania, tunampenda Rais Dk.Samia na tunaendelea kumuunga mkono na kushirikiana naye bega kwa bega wakati wote, kwasababu ya uongozi wake bora kwa Watanzania katika kuwaletea maendeleo.

"Pia, tunaliunga mkono Bunge letu, chini ya Spika wa Bunge, Dk.Tulia Ackson kwa kazi kubwa ambayo limeendelea kuifanya ya kuwaongoza vyema wabunge na kuishauri serikali katika maamuzi mbalimbali ya maendeleo jambo ambalo limeendelea kuleta tija na mafanikio zaidi," alisema.

Kuhusu kauli ya Chifu, Nsingwa wa Mkoa wa Mwanza kuhusu Bunge, alisema UMT, hawakubaliani na kauli hiyo, ambayo inalenga kuwachonganisha Umoja wa Machifu na Wabunge jambo ambalo halipendezi na halina afya Kwa maendeleo ya Taifa.

"Umoja wa Machifu Tanzania (UMT), tunajitenga na kauli ya Chifu Nsingwa, kwani ni yake binafsi, hakutumwa na umoja wa Machifu, kwani sisi tunaheshimu muhimili wa bunge na kuilinda umoja wetu wa wakati wote, tunaheshimu maamuzi ambayo wamekuwa wakifanya wakati wote," alisema.