NA JESHI LA POLISI, DAR ES SALAAM
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watu watatu kwa tuhuma za kujeruhi na kupora watu vitu mbalimbali katika daraja la salenda eneo la mikoko.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP. Muliro J. Muliro, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ufuatiliaji mkubwa wa wahalifu wanao jihusisha na matukio ya namna hiyo.
Aidha Polisi wanaendelea na ufuatiliaji wa wahalifu wanaopora kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jiji na Polisi itawakamata na baadaye kuwafikisha katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.