Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliofanyika katika Kata ya Kaselya, wilayani Iramba, mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga). |
Na HEMEDI MUNGA
Uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, umemuibua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, kuwataka watanzania kuenzi falsafa za wasisi wa Chama.
Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Kaselya, wilayani humo ambapo Mwenda amesema waasisi wa Chama walikianzisha kwa malengo ya watu kuwa wa wamoja katika nchi moja.
Ameeleza kuenzi falsafa hiyo ni watanzania kuendelezaa umoja, mshikamano na upendo katika Taifa lao.
Ameeleza kwa namna yoyote mwananchi akizunguka Tanzania lazima akitazame Chama cha Mapindunzi ambacho kimetengeneza jamii ya watu wanaojitambua, kuheshimiana, kushirikiana na kupendana.
Kuhusu Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Mwenda aliwaomba wananchi mkoani humo kumchagua Rais huyo kwa asilimia 100 katika Uchaguzi Mkuu waa mwaka 2025 aendelee kuwa kamisaa wa kuwasimamia wananchi wa Iramba katika kuwaletea maendeleo.
Amesema Rais Dk. Samia ametekeleza kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na tangu uhuru wa nchi kuwaletea maendeleo waananchi wa wiilaya hiyo.
Mwenda pia aliwataka wananchi kuhakikisha wanachagua wenye viti wa serikali za mitaa wanaotokana na CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumzia sekta ya afya, DC Mwenda, amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia wilaya hiyo imezindua vituo vya afya vipya saba.
Ameeleza lengo la Rais Dk. Samia na maelhuyo ikiwemo maelekezo ya Ilani ya Chama hicho ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya.
Aliongeza, wameboresha Hospitali ya Wilaya ya Iraamba ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa tiba vya kisasa tofauti na awali ambapo wananchi walilazimaka kufuata huduma hizo mkoani Dodoma.
Ameeleza Zahanati 13 zimejengwa ambapo lengo ni kila kijiji kati ya vijiji 70 vya wilaya hiyo kupata zahanati.
Kuhusu umeme, Mwenda, amesema wilaya hiyo ilikuwa na vijiiji 50 vyenye umeme lakini sasa vijiji vyote 70 vimefikiwa huku vitongoji 184 vinaumeme kati ya vitongoji 390 .
Amesema kuna miradi 12 mikubwa ya maji inayoendelea kutekelezwa katika wilaya hiyo, hivyo changamoto ya maji haitakuwepo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Innocent Msengi, amesema alisema Baraza la Madiwani lipo salama, halina makundi na limeungana tayari kwa kufanyakazi, hivyo shughuli za maendeleo katika kila kata zinaendelea vizuri.