UWT WAMSHUKURU NA KUMPONGEZA RAIS DK. SAMIA KWA UONGOZI BORA
VIONGOZI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM mkoani Singida, wamemuahidi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kumchagua kwa kishindo ifikapo 2025 kwa sababu aliyowafanyia ni makubwa.
Akizungumza katika Kongamano la kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia, kwa uongozi bora na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, lililofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mjini Kiomboi mkoani hapa, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, (UWT) ambae anawawakilisha wanawake wa mkoa huo, Grace Mkoma alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesababisha wanawake hivi sasa wanajidai huku wakinababa wakikaa nyuma yao.
"Ndugu zangu Rais wetu ametuheshimisha sana, ametufanya wanawake tutembee kifua mbele, ninampongeza sana Mama yetu, tunakuahidi kukupa maua yako ifikapo 2025," ameahidi Grace.
Aidha, amebainisha kuwa wakati wa nyuma walikua wakisoma kwa kutumia mwanga wa kibatali lakini leo hii umeme umefika kila pahali ikiwemo barabara ya lami kufika mpaka mlangoni kwao.
Mbali na hayo, Grace aliongeza kuwa wanawake wa wilaya na mkoa huo, walikua na shida ya maji lakini leo hii kunamabomba majumbani kwao.
"Hakika hii ni kazi ambayo imefanywa na Mwanamke wa shoka Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hivyo tunakila sababu ya kujivunia mwanamke huyu kwa kutuheshimisha na kusimama kweli kweli:
"Nina kila sababu ya kusema Rais Dk. Samia anatosha na 2025 wanawake wa mkoa wa Singida tunakwenda na Samia kumpa mitano tena," amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Grace amemshukuru na kuompongeza Mbunge wa jimbo hilo, ambae ni Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba kwa kulisemea jimbo hilo, hatimaye likapata fedha zilizoleta maendeleo makubwa.
"Mbunge wetu ni baba wa watoto wengi, kaka wa wadogo wengi na mlezi wa wengi, hakika yeye ni baba mwema sana, hivyo naye tutampa mitano tena," amesema.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa UWT mkoani hapa, Martha Kayaga aliushukuru uongozi wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali unaoongozwa na Dk. Albina Chuwa kwa kuendelea kutekeleza agizo la Rais Dk. Samia kutoa mafunzo ya usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 kwa mkoa wa Singida.
Amesema mafunzo hayo yanawaelimisha namna bora ya kutumia matokeo hayo kwa lengo la kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
Mbali na hayo, kwa sababu wao ni viongozi yatawasaidia kuandaa bajeti na ratiba za kazi zao za kila siku ikiwemo uandikishaji unaoendelea.
Aidha, aliahidi kuwa watayatumia mafunzo hayo hususan katika kipindi hichi ambacho wanaendesha uandikishaji kidigitali kujua takwimu kutokana na visimbuzi wanavyotumia.
![]() |
| Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Kayaga, katika kongamano hilo. |
Reviewed by Gude Media
on
March 23, 2024
Rating:


