IRAMBA - SINGIDA.
Waziri wa Fedha, ambae ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dk. Mwigulu Nchemba, amewaeleza wananchi kuhusu uwekaji wa madaraja kwa sasa sio jambo la ajabu chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, sababu yapo madaraja mengi yanajengwa kufuatia fedha zinazotolewa kukamilisha miradi hiyo.
Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo na kuwahakikishia wananchi wa kata ya Ndago wilayani Iramba mkoani Singida kuwa kabla ya Bunge la bajeti kuisha, Mkandarasi atakua amekwisha pata fedha, hivyo kuanza ujenzi wa barabara hiyo.
Aidha, ameeleza ujenzi wa barabara ambayo inaanzia Kizaga kupitia Kata ya Mukulu, Ndago, Mbelekese, Kaselya mpaka Singida mjini itaendelea kufungua uchumi wao.
"Ndugu zangu, hapa Ndago panakua mjini kwa sababu lami itapita hapa, hivyo yale madaraja yote yaliopo katika barabara hiyo yatafanyiwa kazi, kabla ya mwezi wa saba mwaka huu tutampatia Mkandarasi fedha aanze kazi mara moja, " amesema.