WANANCHI WA GEITA MJINI WAMFAGILIA MBUNGE KANYASU KWA UFUATILIAJI WA CHANGAMOTO KUZIPATIA UFUMBUZI

Na MWANDISHI WETU

WANANCHI wa Jimbo la Geita Mjini,  wamempongeza mbunge wa Jimbo hilo, Costantine Kanyasu kwa jitihada kubwa za kuwaletea maendeleo na utatuzi changamoto za wananchi.

Wananchi wametoa pongezi hizo, jimboni humo Mkoani Geita katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini, huku wakimpongeza kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake na Samia, Mkoa wa Geita, Adelina Kabakama, alisema Mbunge Kanyasu anafanya kazi kubwa, huku na wao wakishirikiana naye katika maeneo mbalimbali hususan ni pale wanapo mhitaji.

Vilevile, Esta Maphole (60), amemshukuru Mbunge Kanyasu kwa upendo wake kwa wananchi na namna anavyoshirikiana vyema na wananchi hususan katika kutatua kero zao ikiwemo  migogoro ya madini  huku, mjasiriamali wa upishi wa chakula,  Anna Benedict, akiwataka wananchi kuendelea kumpa ushirikiano mbunge huyo na kumwombea afya njema.