KANYASU AMFAGILIA DK. BITEKO KUFIKISHA NISHATI YA KUTOSHA GEITA MJINI

Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Jimbo la Geita Mjini, Costantino Kanyasu amempongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuimarisha nishati nchini hususan jimbo hilo kuhakikisha kata zote 13 zitapata nishati ya umeme.

Kanyasu ameyasema hayo mkoani Geita, jana, katika mkutano wa ufunguzi wa maonesho ya saba ya Teknolojia ya madini, yaliyo udhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Dk.Biteko.

Kanyasu amesema Dk.Biteko amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha nishati inapatikana nchini ambapo katika jimbo la Geita Mjini wamepata umeme wa kutosha katika kata 13 na vijiji 65.

"Kiukweli Geita, tunakushuru kwa kazi kubwa unayofanya ya kuhakikisha nishati inapatikana na kuondoa changamoto za wananchi katika nishati ya umeme hapa Geita, kata zote zina umeme ni maeneo machache tu ambayo nayo yanaendelea kushughulikiwa kwani wakandarasi wako site wakiendelea na matengezo," amesema.

Aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Dk. Samia katika jitihada kubwa wanazozifanya za kuleta maendeleo kwa wananchi likiwemo suala la nishati na kuwataka kuitaunza miundombinu hiyo muhimu.