TAASISI ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimataifa ikiwemo Bodi ya Kimataifa wa Utafiti wa Saratani kutoka Marekani na wataalamu wa Zambia, kuhakikisha wanaendeleza utafiti kubaini tiba ya saratani mbalimbali.
Pia, ameishukuru serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa ORCI, ikiwemo maabara ya kisasa ambayo imeendelea kusaidia katika tafiti mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk.Julius Mwaisalage, jijini Dar es Salaaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wadau wa utafiti kilicho fanyika hospitalini hapo, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORC).
"Tumekuwa hapa na taasisi ya utafiti kutoka Marekani na Zimbabwe, lengo ni kufanya tathmini ya visababishi vya saratani na namna ya kuzuia kwake, kujenga uwezo kwa wataalamu njia bora zaidi ya kutibu, hususan saratani zinazohusiana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (HIV)," amesema.
Akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Wizara ya Afya, Meneja wa mpango wa damu salama, Abdu Juma, amewapongeza ORCI na Bodi hiyo ya utafiti wa saratani kwa kikao hicho na kuwezesha uwekezaji mkubwa katika maabara ya utafiti iliyopo katika Taasisi hiyo.