BALOZI DK. NCHIMBI AKAGUA UJENZI WA JENGO LA CCM MKOA WA SINGIDA

 SINGIDA 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amekagua  ujenzi wa jengo la CCM Mkoa wa Singida.

Dk. Nchimbi amekagua ujenzi huo leo wakati wa ziara yake mkoani humo ambayo ilianza Mei 29 na kukamilika  Mei 30, 2024.

Aidha,  ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama mkoa, Martha Mlata.

Jengo hilo ni moja kati ya majengo yaliwekwa jiwe la Msingi Mei 03, 1986 na Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikua mwenyekiti wa kwanza wa CCM.