Mbunge Jimbo la Madaba, Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea Vijijini Dkt. Joseph Mhagama, akiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wametembelea eneo la ujenzi wa nyumba ya mhitaji, anayojengewa na Taasisi ya Tulia Trust katika Kata ya Lituta Kijiji cha Mtepa.
Nyumba hiyo inayojengwa kupitia mpango wa 'Tulia Trust Mtaani Kwetu', itakuwa nyumba ya 13 kujengwa kwa kuwasaida wanaoishi katika mazingira magumu.
Nyumba hiyo ni ya kwanza kujengwa katika Mkoa wa Ruvuma, licha uwepo wa wahitaji wengine wanao saidiwa kupitia taasisi hiyo.