Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida kimevuna wanachama 50 kutoka CHADEMA wakiongozwa na aliyekua Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Singida Vijijini.
Wanachama hao wamerudisha kadi za chama hicho na kuchukua kadi za CCM huku wakipokelewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi wakati wa mkutano wa hadhara katika viwanja vya Bombadia mjini hapa.
Mbali na hao, wanachama wapya 50 wamejiunga na CCM, hivyo kufanya idadi ya wanachama kufikia 100 ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa ya ziara ya Balozi Dk. Nchimbi aliyoianza mwezi Mei 29 na kutarajiwa kuisha Mei 30.