BALOZI DK. NCHIMBI AMEANZA ZIARA YA KUKAGUA UEKELEZAJI ILANI YA CCM MKOANI SINGIDA

 


MANYONI - SINGIDA 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amepokelewa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Singida, Martha Mlata.

Balozi Dk. Nchimbi ameanza ziara hiyo, leo Mei 29 kwa lengo la kuendelea kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ya mwaka 2020 hadi 2025 ambapo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameleta miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kuendelea kuwahudumia wananchi.

Aidha, ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Ziara hiyo, imeanza leo Mei 29 na inatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 30, 2024.