IRAMBA - SINGIDA
Mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amewatahadharisha viongozi wa kisiasa wanaodaiwa kutumia kauli za kichochezi kuwa wanao wajibu wa kulilinda Taifa hii.
Mwenda ametoa tahadhari hiyo, leo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo katika Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, yaliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mjini Kiomboi.
Aidha, amewasihi viongozi wote ikiwa ni waziri, Katibu Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Madiwani, Venyeviti wa vijiji na watumishi wa umma ngazi zote kuwa wanao wajibu wa kulilinda Taifa hili.
Amesema wanapaswa kumuiga kwa kivitendo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambae anajitahidi kwa hali na mali, usiku, mchana, masika, kiangazi, iwe jua au mvua yupo barabarani halali wala hapumziki kwa kulipigania Taifa hili lipate maendeleo.