Kilave awataka viongozi wa vyama vya siasa Temeke kumuunga mkono Rais Dk. Samia

Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Jimbo la Temeke,  Dorothy Kilave, amewataka viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Temeke, kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwani amefanya kazi kubwa ya kuimarisha utengamano wa kisiasa na kuimarisha miradi mingi ya maendeleo jimboni humo.

Kilave ameyasena hayo jimboni humo, alipokukutana na kuzungumza na viongozi kutoka vyama 15 vya siasa Temeke.

"Rais Dk.Samia ameimarisha hali ya kisiasa nchini kupitia 4R, imeleta utengamano wa kisiasa hivyo hatuna budi ya kukaa pamoja na kumuunga mkono kwa mafanikio makubwa aliyoyafanya jimboni kwetu,"amesema.

Mbunge, Kilave amewataka viongozi hao kuendelea kuhamasisha jamii juu ya kujiandikisha katika daftari la mpiga kura, wapate sifa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi  Mkuu.