ZUNGU AWATAKA VIONGOZI WA CCM KATA YA KIVUKONI KUEPUKA MALUMBANO NA UGOMVI NA BADALA YAKE WASHIRIKIANE KULETA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (kushoto), akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule, alipowasili katika ukumbi wa Karimjee, kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa CCM Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam.

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, wakati wa mkutano huo Karimjee, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kivukoni, Peter Mbawala.

Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule, wakati wa mkutano huo, pamoja na kuwatakia heri ya Sikukuu ya Christmass na Mwaka Mpya 2023.





 

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Ilala, Naibu Spika Mussa Zungu, amewata wajumbe wa mkutano wa viongozi wa CCM Kata ya Kivukoni, kuepuka malumbano na ugomvi.

Zungu alisema hayo, Dar es Salaam, jana, wakati wa mkutano huo wa kutakiana heri ya Sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya 2023, ambapo alisema hakuna sababu ya kulumbana na ugomvi.

Alisema  hakuna sababu ya kugombana na wanaogombana katika Chama cha Mapinduzi (CCM), hawajawiva katika Chama.

"Mwaka Mpya lazima uwe na mambo mapya, hivyo tuepuke  malumbano na magovi na misukosuko isiyokuwa na afya katika Chama chetu, kugombana pasipo uchaguzi ni udhaifu", alisema.

Zungu alisema kama hujalizika na maamuzi ziko njia za Chama zimewekwa kuna kanuni na endapo umeona umeonewa fuata taratibu ziliwekwa na hakuna sababu ya kugombana.

Alisema wanauchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025, uchaguzi utakuwa mgumu, ni vizuri kushirikiana na kupendana ili watimize malengo ya Chama kushika dola.

Kwa upande wa Diwani wa kata hiyo, Sharik Choughule, amewashukuru viongozi hao kwa kushirikiana nao na kusaidia kuleta maendeleo katika Kata ya Kivukoni.

Alisema kata yao bado ina baadhi ya changamoto na kwamba kwa kushirikiana nao anaamini zitaondoka na maendeleo yatapatikana.

"Nawashukuru kwa kunipa lidhaa ya kuongoza kata hii na ushirikiano mnaonipa na mimi lazima nihakikishe maendeleo yanapatikana katika kata yetu, pia namshukuru Mbunge wetu wa jimbo la Ilala Zungu, tunashirikiana vizuri", alisema.

Pia endapo kuna tatizo naomba mniite na miambie tuweze kuondoa hilo tatizo kwa yeye yupo kuwatumikia wananchi wote hususan wa Kata ya Kivukoni kwa lengo la kuleta maendeleo.