JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO (JWK), IMEZINDUA VITAMBULISHO MAALUMU VYA KUWATAMBUA

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Chalangwa Makwilo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Jumuiya ya Wafanya Kariakoo (JWK), Kusirie Mwasha, kitambulisho cha jumuia hiyo, Dar es Salaam, jana. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa JWK, Martin Mbwana na Makamu Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Yahaya Ally.

Wanachama ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa vitambulisho vya jumuiya hiyo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Chalangwa Makwilo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Dharura ya Jumuiaya ya Wafanya Kariakoo (JWK), Hamidu Maftaha, kitambulisho cha jumuia hiyo, Dar es Salaam, jana. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa JWK, Martin Mbwana na Makamu Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Yahaya Ally. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Martin Mbwana, akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa vitambulisho vya wafanyabiashara Kariakoo, Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu na kulia ni Mkuu wa Polisi  Wilaya ya Kariakoo, William Solla.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu, akizungumza akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya jumuiya hiyo.

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana, ameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwa na timu mmoja ya ukaguzi wa kikodi Kariakoo.

Mbwana alisema hayo, wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya kuwatambua wafanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam, jana.

Alisema kuwekuwa na timu nyingi za ukaguzi na kusababisha usumbufu kwa wafanyabiashara pindi mizigo yao inaposhikiriwa na TRA.

"Mfanyabiashara mmoja anakaguliwa na maofisa wa TRA zaidi ya mmoja kutoka maeneo mbalimbali, ushauri wetu kama jumuiya ya wafanyabiashara Kariakoo, TRA iwe moja itakayosimamia eneo lote la Kariakoo", alisema.

Mbwana alisema suala la kuwa na timu nyingi za ukaguzi inaweza kusababishwa kuwepo kwa rushwa na ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya vijana wa mamlaka hiyo.

Pia Mbwana alisema ikitokea mfanyabiashara mwenyekitambulisho ya jumuiya amepata shida, ameomba mamlaka zimtambue na wampe ushirikiano au huduma anayohitaji.

Naye Mwenyekiti wa Machinga Kariakoo, Stephen Lusinde, amempongeza Rais Dk. Saimia Suluhu Hassan, kwa kuwaondolea kikwazo katika suala ulipaji kodi.

Alisema kitendo cha Dk. Rais Samia kuruhusu mfanyabiashara anapoanza biashara yake, kuzungumza na TRA wampe muda wa kulipa kodi za serikali, huku akiendelea na kufanyabiashara, kitawasaidia wao kukua kibiashara na kuweza kulipa kodi za serikali kwa wakati.

"Nichukue fursa hii sisi Wamachinga Taifa na Kariakoo, kumpongeza Dk. Rais Samia, kwa kutuondolea kikwazo hicho, kwani hapo awali unafungua biashara leo na ukienda TRA unaambiwa mambo mengi, ukirudi huendi tena, alisema.

Kwa upande wa Meneja wa TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu, vitambulisho hivyo ni muhimu katika ushirikiano wa TRA na wafanyabiashara wa Kariakoo.

Alisema hilo ni daraja zuri la kushirikiana pande zote mbili katika kutatua changamoto zilizopo baina ya TRA na wafanyabiashara.

Katundu alisema kitambulisho hicho ni utambulisho tosha utakaosaidia endapo kutatokea changamoto baina yao ni rahisi kuwafahamu kwa kuwapata.

"Kwa changamoto ndogo tunaweza kukuacha ukaendelea na kufanya biashara na endapo tutakuhitaji ni rahisi kukupata, kupitia Jumuiya ya Wafanyabiashara Karikoo, tukajadiliana kwa kutatua hizo changamoto", alisema.

Pia Katundu alisema baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao, ataziwasilishwa kunakohusika ili zifanyiwe kazi ikiwemo kukutana na viongozi wao.