TAASISI ZA ELIMU ZAPATA MSAADA WA DOLA 20,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido (kulia), akikabidhi msaada wa hundi ya dola za Kimarekani 10,000 zilizotolewa na  shirika la Nos Vies en Partage Foundation ((NVeP),  kwa Mkurugenzi wa mipango kutoka taasisi ya TanSAF, Alex Elifas, Dar esSalaam. Kutoka kushoto ni wanafunzi waliopo katika programu za taasisi hiyo, Bruno Basley Bruno na Isaya Charles.  Shirika la  Nos Vies en Partage Foundation, linafadhiliwa na Rais na afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido (kulia), akikabidhi msaada wa hundi ya dola za Kimarekani 10,000 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilosa, Wapa Mpwewe (wa pili kulia) kwa niaba ya Shule ya Sekondari ya Parakuyo, aliongozana na viongozi wa shule hiyo, Dar es Salaam, jana. Msaada huo umetolewa na Shirika la Nos Vies en Partage Foundation, linafadhiliwa na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.

 

Shirika la  Nos Vies en Partage Foundation (NVeP) na  Kampuni ya Barrick, wametoa msaada wa dola za 20,000 Marekani, kwa taasisi  isiyo ya Serikali ya Tanzania Student Achievement Foundation (TanSAF) na Shule ya Sekondari Parakuyo ya mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa kukabidhi feha hizo, Dar es Alaam, Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, amesema kila robo ya mwaka, taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja  kwa  moja kwenye jamii zenye uhitaji.

Ngido amesema  fedha hizo ni kusaidia  kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu.

Amesema msaada huo umetokana na fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage Foundation (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.

Ngido amesema shirika hilo limekuwa likisaidia makundi maalumu kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

“Hadi sasa tumetoa msaada kwa zaidi ya mashirika 10 Tanzania kupitia taasisi ya NVeP, lakini huu ni mwanzo leo tuko hapa kuleta mabadiliko katika taasisi mbili kwa kuzipatia msaada  wa dola za kimarekani 10,000  kila  moja kwa ajili ya kuboresha elimu kwa watoto’’, amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mipango wa  taasisi ya TanSAF, Alex Elifas, amesema msaada huo utasaidia kuwatafutia wenye vipaji kutoka familia zisizo na uwezo  wa kifedha kutafutiwa fursa ya kusoma katika baadhi ya vyuo vikuu bora duniani kote.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilosa, Wapa Mpwewe, alipokea hundi kwa niaba ya Shule ya Sekondari Parakuyo, alisema feha hizo zitasaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ya shule hiyo.

“Kwa bahati mbaya shule hii ilipata uharibifu kwa majengo kutokana na mvua kubwa za mafuriko mwaka jana, fedha hizi zinatasaidia kujenga upya nakuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu”, amesema.

Mmoja wa wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, Bruno Bruno, mhitimu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kisimiri, iliyopo mkoani Arusha, amesema yuko katika mchakato wa kwenda kusoma elimu ya chuo kikuu nchini Marekani, baada ya kusaidiwa kutafuta chuo na shirika la TanSAF.