Na Mwandishi Wetu
Mwenge wa Uhuru umeendelea na mbio zake mkoani Dar es Salaam, ambapo umeingia wilayani Kinomdoni na kutembelea miradi saba yenye thamani ya sh. bilioni 74.5.
Akipokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, ametaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA).
Amesema mradi huo uliopo Mtaa wa Kihonzile Kata Wazo, umedhaminiwa na Benki ya Dunia na unathamani ya sh. bilioni 71.
Mtambule, ameeleza miradi mingine ni klabu ya upingaji rushwa katika Shule ya Msingi Mabwepande, upandaji miti katika Gereza la Wazo na uwekaji jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa nje katika Zahanati ya Mabwepande.
Pia miradi wa kikundi cha ujasiriamali (KIUWA), kutembelea shughuli za lishe katika Shule ya Sekondari Daniel Chongolo, na miradi ya usambazaji wa gesi majumbani unaotekelezwa na TPDC.
Mtambule ametaja mradi mwingine ni ujenzi wa Barabara ya Mkalama Kata ya Ndugumbi yenye urefu wa kilomita 0.8.
“ Mradi mwingine ni uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa , matundu 22 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Kumbukumbu,”alieleza Mtambule.
Amesema miradi yote hiyo inajumla ya thamani y ash. bilioni 74 . ambazo zimetolewa na serkali binafi na mapato ya ndani ya hamashauri hiyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu, alipongeza viongozi wa Wilaya ya hiyo na watendaji kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.
"Katika miradi huu wa maji wa DAWASA barabara ya Mwenge wa Uhuru, umekagua nyaraka za ujenzi ziko vizuri. Pia umekagua mradi wenyewe uko vizuri ."alisema Kaimu.
Kaimu alisitiza uwajibikaji, kupiga vita rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya Maralia, Ukimwi, kuzingatia lishe bora na kutunza mazingira.
Mwenge wa Uhuru tayari umetembelea Wilaya za Temeke, Kigamboni, Ilala, Ubungo ambapo kesho utaendelea na mbio zake Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar.