NDJEMBI ASHAURI KINONDONI KUWA NA SHULE YA RAIS YA RAIS SAMIA


Na Mwandishi Wetu

 Naibu  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi, ameeleza kukoshwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya elimu katika Wilaya ya Kinondoni  na kushauri wilaya hiyo na Mkoa wa Dar es Salaam, kuwe na shule yenye jina  la Rais Dk. Samia Suluhu Hassam.

Ameyasema  hayo Dar es Salaam, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule za sekondari na msingi .

Amesema   nchi nzima Rais Dk. Samia ametoa zaidi ya bilioni sh. 200 kujenga na kukarabati  miundombinu ya elimu ambapo kwa kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee ametoa sh. bilioni  7  kupitia mradi wa BOOST wa kuboresha elimu ya msingi na sh. bilioni 9.9  katika Mpango wa Kuboresha Elimu ya Sekondari.

“ Kinondoni au Mkoa wa Dar es Salaam, jengeni shule na ipeni jina la Rais Dk. Samia. Kwakweli amefanya kazi kubwa katika kuboresha elimu,”amesema Ndejembi, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule, aliahidi kutekeleza ushauri huo.