RC CHALAMILA AZINDUA UPIMAJI AFYA NA MATIBABU BURE


Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila,   amezindua   kambi za huduma ya upimaji afya na matibabu bila malipo  Afya Check, katika Shule ya Msingi Mbagala Rangi Tatu, wilayani Temeke.

Chalamila amesema kambi hizo zitafanyika katika wilaya zote tano za mkoa wa Dar es Salaam, lengo kuwafikia wananchi 20,000.

Uzinduzi huo umefanyika  Mbagala katika Shule ya Msingi Mbagala Rangi Tatu, wilayani huo na kuhudhuriwa na umati wa wananchi kupima afya zao na kupatiwa matibabu.

Chalamila amesema, upimaji afya na matibabu bure  utafanyika kwa siku 10 katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Kinondoni, Ubungo na Ilala.

 Amesema magonjwa yatakayo husika ni saratani, moyo, shinikizo la damu, Ukimwi,  chanjo  dhidi ya Uviko 19, chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano ambao hawakupata chanjo hiyo au hawakumaliza.