WATOTO 200 KUFANYIWA TOHARA BURE DAR


Na Mwandishi Wetu

Mamia ya wananchi wamejitokeza kuwafanyia tohara watoto wao katika Kituo cha Afya cha The Sun Shine Muslims Volunteers (SMV)  kilichopo Ilala  Gereji, Dar es Salaam ambacho kinaendesha kampeni ya tohara kwa watoto bila malipo.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa SMV Dk. Juma Mwimbe watoto 200  wenye umri wa mwaka 1-12 kutoka familia zenye mahitaji maalumu wamelengwa kufanyiwa tohara hiyo bure

“Leo pekee tumepata watoto 180. Bado wanaendelea kujitokeza. Tohara ni suna  ya Mtume Muhammad (S.A.W) na ni usafi unamuepusha mtu kupata maradhi mbalimbali,”anasema Dk. Mwambe na kuhimiza  jamii kushirikiana na kituo hicho.