MJEMA KUANZA ZIARA YA SIKU SABA DAR ES SALAAM



Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Itikadi,  Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema,  anatarajia kufanya ziara ya siku saba katika Mkoa waa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Katibu wa Siasa na Uenezi  wa CCM mkoani humo, Ally Bananga,  ziara hiyo inaanza  kesho.

Banaga amesema Mjema, atakutana na  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa na Wajumbe wa jumuiya zote tatu za Chama ambazo ni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),  Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Vijana (UVCCM).

 Amesema, Mjema atakutana na wajumbe hao katika  ukumbi wa  Anatoglou ambapo kikao hicho pia kitajumuisha makada wa CCM watakaoandaliwa.

Bananga amesema, Agosti 24, Mjema atafanya ziara Wilaya ya Kigamboni na Agosti 25, Wilaya ya Ubungo, Agosti 26, wilayani Ilala na Agosti 27, atahutubia mkutano wa hadhara wilayani Temeke. 

Amesema mkutano huo utahutubiwa pia na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mohammed Kawaida na kuwataka wanachama kujitokeza kwa wingi.

Banga, amesema  ziara hiyo itaendelea Agosti 28 katika Wilaya ya Kinondoni na kuhitimishwa Agosti 29 katika Wilaya ya Temeke.

Amesema katika wilaya hizo tano za Mkoa wa Dar es Salaam,  Mjema atakutana na wajumbe wa Halmshauri Kuu za Wilaya, Mabaaraza ya jumuiya zote  za wilaya na wadau walioandaliwa kwa ngazi husika.