Na Mwandishi wetu
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema wamesahau matokeo ya Tanga na wanaanza mazoezi kuhakikisha wanatoa kichapo kikubwa katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu.
Yanga walishindwa kutetea taji la Ngao ya Jamii baada ya kufungwa penalti 3-1 dhidi ya watani wao Simba kufuatia kumaliza dakika 90 bila kufungana, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
“Hatupaswi kuweka kichwani matokeo mabaya ambayo tuliyapata, hasira zote tunazielekeza katika Ligi Kuu, tunaanza na KMC, tutafunga mabao mengi kuhakikisha tunakaa kileleni kuanzia mchezo wa kwanza,” amesema.
Kocha huyo amewaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuwasapoti kila wanapocheza kuweza kuwapa hamasa wachezaji wafanye vizuri.