MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA SH. BIL 4.15 IRAMBA-DC MWENDA



 IRAMBA - SINGIDA 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Suleiman Mwenda, ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba na kuahidi kuulinda na  kuukimbiza katika wilaya hiyo.


Mwenda amesema Mwenge wa Uhuru utakagua  Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya sh bilioni 4.15  wilayani hapa.


Aidha, amesema kuwa Wananchi wote wako tayari kuusherehekea Mwenge wa Uhuru katika maeneo yao kwa kuwa wamejitokeza kwa wingi kila kona.


Mwenge wa Uhuru umepokelewa  Wilayani Iramba katika viwanja  vya Malendi Tarafa ya Shelui wilayani hapa leo Septemb 22 mwaka huu.