Mongella: CCM ndiye ‘Baba’ wa demokrasia nchini

Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, kimefanya kazi kubwa na yenye mafanikio makubwa. Hii ni kutokana na juhudi za Rais Dk. Samia pamoja na viongozi wengine wa chama hicho. Ni muhimu kupongeza na kumshukuru kwa juhudi zake, lakini zaidi ya hayo, tunapaswa kumuunga mkono katika juhudi zake za kuleta maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella, tarehe 7 Septemba 2024, wakati akizungumza katika Halmashauri ya Msalala, Kahama, mkoani Shinyanga, katika ziara yake ya siku 7 mkoani humo. Mongella alisisitiza kuwa CCM ndiyo muasisi wa demokrasia na dhana zote za utawala bora nchini Tanzania.

Mongella pia alielezea falsafa ya Rais Dk. Samia ya 4R: Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding). Aliwahimiza wananchi na wanachama wa CCM kuishi falsafa hiyo, sio tu ndani ya chama, bali pia majumbani, vitongojini, vijijini, na mitaani ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani.