KINANA AHIMIZA SERIKALI KUHARAKISHA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, akikagua maeneo yaliyoathirika na maafriko katika Kijiji Cha Muhoro, alipokwenda  kuwapa pole wakazi wa Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. (Picha zote na Fahadi Siraji CCM).

 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, amesema msaada mkubwa wa haraka unahitajika kwa wananchi  walioathirika na mafuriko wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Amesema hayo baada ya kupokea taarifa na kushuhudia hali ilivyo wilayani humo, ambapo kata 12 kati ya 13 zimeathirika na kuitaka serikali kuharakisha misaada ikiwemo chakula na malazi kwa zaidi ya watu 88,000 walioathirika.

Kinana ametoa wito huo leo, Aprili 9, 2024, alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Muhoro na Chumbi, baada ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo, yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Mto Rufiji kufurika katika makazi ya watu.

"Nimezungumza na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa namna nilivyojionea na nimemweleza uharaka wa mahitaji, sina shaka hata kidogo na yeye atakuja kujionea. Haraka ameitisha kikao na mawaziri wote wanaohusika na maswala ya maafa, nina hakika akishakuja hapa kasi ya kutoa huduma itaanza kwani kwa sasa ni ndogo sana,” amesema.

Kinana amesema kutokana na hali hiyo serikali iongeze juhudi za kutoa huduma kwa wananchi waliopatwa na maafa hayo ambayo yameathiri pia shule na zahanati.

“Nimekuja kuwapa pole kwa niaba ya Rais, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nimekuja kujionea hali ilivyo, lakini niendelee kutumia fursa hii kuihimiza serikali kuleta misaada haraka kwa wananchi walioathirika," amesisitiza Makamu Mwenyekiti Ndg. Kinana.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, Akikagua maeneo yaliyoathirika na maafriko katika Kijiji Cha Muhoro, alipokwenda  kuwapa pole wakazi wa Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani waliokumbwa na mafuriko.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, Akikagua maeneo yaliyoathirika na maafriko katika Kijiji Cha Muhoro, alipokwenda  kuwapa pole wakazi wa Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, akikagua eneo la Shule ya Msingi Muhoro  katika Kijiji Cha Muhoro, alipokwenda  kuwapa pole wakazi wa wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, waliokumbwa na mafuriko. 


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza na wananchi wa vijiji vya Muhoro na Chumbi, baada ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo,  yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Mto Rufiji kufurika katika makazi ya watu.