Na MWANDISHI WETU
KASI ya utendaji ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imezidi kupamba moto katika Kata ya Vingunguti, jijini Dar es Salaam hususan sekta ya afya, baada ya Rais kutoa vifaa vya kipimo cha Utra Sound na huduma ya kinywa na meno katika Zahati ya Vingunguti.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata hiyo, amesema licha ya huduma hizo pia Rais Dk. Samia, ameeleza gari la kubebea wagonjwa ambalo (Kumbilamoto) alifadhili litumike maalumu katika Zahanati hiyo .
Kumbilamoto amesema, gari hilo pia litabeba maiti bila malipo kwa wakazi wa Vingunguti mahari popote katika Mkoa wa Dar es Salaam, kuwapunguzia gharama za maziko wananchi.
“Tunamshukuru Rais Dk. Samia, Utra Sound inafungwa katika Zahanati ya Vingunguti. Pia ametuongezea huduma hapa ya kinywa na meno kwa gharama nafuu", amesema Kumbilamoto.
“Ambulance hii nilifadhili miaka ya nyuma. Ilikuwa ikitumiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Lakini Rais Dk. Samia, ametoa magari 10 ya kubebea wagonjwa katika halmashauri yetu, hivyo gari hili limerudi Zahanati ya Vingunguti. Licha ya kubeba wagonjwa pia tumeliongezea majukumu ya kubeba wapendwaa wetu watakaofariki na litatoa huduma bila malipo kwa wakazi wa Vingunguti,”