MJUMBE WA KAMATI YA SIASA CCM MKOA WA SINGIDA AMEWATAKA UVCCM KUNADI SERA ZA CHAMA KOKOTE WALIKO

IRAMBA- SINGIDA

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida ambae ni Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego amewataka  Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) wa mkoa huo kuwepo popote ikiwemo aridhini, angani na mitandaoni kunadi sera za CCM.

RC Halima ametoa  wito huo leo, wakati akiongea na wajumbe wa Baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani hapa.

Aidha,  amewataka kuzungumzia manufaa ya CCM na serikali yake ikiwemo kujiandaa na  kugombea katika serikali za mitaa kwa sababu ndio msingi na mtaji wa CCM.

"Nendeni mkajipime, nataka kuona wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa serikali za mitaa wanatokana na vijana wa CCM," ametoa wito.