RC DENDEGO AWAONGOZA WANANCHI WA IRAMBA KUFANYA USAFI



IRAMBA - SINGIDA 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amewaongoza wananchi wa wilaya ya Iramba kufanya usafi wa mazingira.

Dendego amefanya zoezi hilo leo, katika eneo la dampo liliyopo mjini Kiomboi wilayani hapa mkoani humu.

Akizungumza na wananchi walioshiriki katika usafi huo, amewashukuru  wanakinama kwa kuwa mstari wa mbele  katika zoezi hilo  huku akiwataka viongozi wa soko la mjini hapa  kuwajibika kikamilifu.

"Ninataka wananchi wakiowemo viongozi wanaofanya kazi maasa 24 kwa sababu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amaeisha elekeza wanakinama, watu wenyewe mahitaji maalumu na vijana kupata mikopo ya asilima 10 ifikapo julai mwaka huu," amesema.