BENKI ABSA YAJA NA MILIKI GARI YA NDOTO YAKO

 


Na TIMOTHY MARKO, Dar es Salaam

KATIKA kuhakikisha Mtanzania anamiliki gari, Benki ya ABSA imenzisha mkopo maalumu wa kumiliki gari la ndoto yake ijulikanayo 'Miliki Gari ya Ndoto yako'.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya ABSA, Lilian Ndabu, amesema benki hiyo imekuja na mkopo gari kumuwezesha mteja wa benki hiyo kumiliki gari.

"Tunamuwezesha mteja kupata Mkopo  Gari ya Ndoto yake kuanzia Sh.milioni 30 hadi milioni 500 kwa kipindi cha miaka mitano", amesema.

Ndabu amesema mteja ataanza kulitumia gari huku akilipa mkopo wake kidogo kidogo.

Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha Mikopo wa Benki ya ABSA, Patricia Nguma, amesema Katika kuhakikisha Mteja wa Benki hiyo anufaika imekuja na mkopo wa Gari ilikuendana na matakwa ya soko.

Amesema mkopo kwa magari yaliyotumika ni asilimia 15 gari jipya ni riba ya asilimia 10.

"Ili uweze kupata mkopo wetu wa gari lazima uwe na akaunti katika benki yetu ya ABSA ", amesema.