Kahyarara - Serikali itaendelea kufanya uwekezaji mkubwa sekta ya uchukuzi kipata wataalamu wa kuendesha miradi ya kimkakati

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara, amesema serikali itaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo, kupata wataalamu wakutosha watakaosaidia kuendesha miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Shirika la Ndege (ATCL) na Mamlaka ya Bandari (TPA), kukuza uchumi.

Kahyarara ameyasema hayo jijini Dar es Salaam,  katika Mahafari ya 23 Chuo Cha Bandari, alipokuwa akiwahutubia wahitimu na wananchi mbalimbali walioudhuria.

“Msukumo wa Wizara ni kuendeleza Taasisi zake zenye vyuo vinavyotoa elimu ya kuzalisha waalamu, kwani hii sekta ndiyo imewekezwa fedha nyingi zaidi zingine kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi,”amesema.

“Serikali itajitahidi kuwekeza sekta ya usafirishaji, hasa Bandari ambayo bado inahitaji uwekezaji mkubwa ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufungua uchumi wan chi,”amesema.