MABEHEWA MAPYA YA SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC) YAMEANZA KUTUMIKA NA ABIRIA WANAOKWENDA KIGOMA

 SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limesema hawatapandisha nauli kwa abiria wasafiri wakati wa kipindi hichi cha Sikukuu za mwisho mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, wakati akizindua  safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, kwa kutumia mabehewa mapya 21 kati ya 22 yaliyowasili nchini hivi karibuni.

Kadogosa amesema, msimu huu wa sikukuu Watanzania wengi  wanakwenda katika mikoa mbalimbali kwaajili ya rikizo na sikuku za Chrismasi na Mwaka mpya, TRC imejipanga  kuhakikisha inawahudumia vizuri zaidi ya mwaka jana.

Amesema TRC haitapandisha nauli na badala yake itaongeza idadi ya safari kutoka mara mbili hadi mara tatu kwa wiki .

“Kama tujuavyo kwa wenzetu wa Kaskazini ni jadi yao kurudi makwao kila mwishoni mwa mwaka kusalimia  na ikifika Januari na Februari  hurejea tena Dar es Salaam kwa wingi, hivyo wasiwe na wasiwasi kuhusu usafiri kwani mwaka huu watakuwa zaidi ya mwaka jana ,” amesema.

Kuhusu Mabehewa mapya 21 yanayokwenda mkoani Kigoma, Kadogosa amesema mabehewa hayo yamefanyiwa kwa mujibu wa sheria na baada ya kupitishwa na Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA),  yamekidhi mahitaji ya kusafirisha abiria.

“ Hatimaye leo tumeanza safari rasmi kwa kutumia mabehewa mapya 21 ya Meter Gauge (MGR) kwenda Kigoma na treni itakaporejea Dar es Salaam, itaanza safari ya kwenda Kilimanjaro ambapo  mabehewa hayo yatasaidia kupunguza  msongamano wa abiria kugombania upatikanaji wa tiketi,” amesema.

Kadogosa amesema mabehewa hayo yalinunuliwa na serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi  katika kutoa huduma ya usafiri wa reli nchini.

Aidha Kadogosa amesema safari rasmi zimeanza baada ya majaribio ya awali  umbali wa  kilometa 400 kutoka Dar es Salaam –Morogoro ambapo LATRA imeridhia mabehewa hayo  kuanza kazi rasmi.

Mabehewa mapya  ya abiria ni 20  ambayo yamebeba jumla ya abiria 1500  wanaotoka Dar es Salaam kwenda Kigoma  huku behewa moja  likitengwa  kwa ajili ya huduma za mgahawa.

 “Kufuatia  ununuzi wa mabehewa  hayo, Shirika hilo limeongeza  idadi ya mabehewa ya treni ya Deluxe kwenda mikoa ya Kaskazini kutoka mabehewa sita hadi 16 na njia ya reli ya kati kutoka  mabehewa 4 hadi 20,” alifafanua.

 Alisema TRC  itaongeza idadi ya mabehewa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu watakaojitokeza kutumia usafiri huo.

Akizungumza na Blog hii mmoja kati ya  abiria waliosafiri na treni hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Sheha Ibrahim,  amesema kuwa mabehewa hayo yako vizuri na yakiendelea hivyo yatavutia watu wengi kutumia usafiri wa treni na kuachana na mabasi.

‘’Nauli ya usafiri huo haijaongezwa  kwani wanatumia za  zamani za treni ya deluxe ambayo kwa daraja la kulala  ilikuwa sh. 65,000 kutoka Dar es Salaam- Kigoma.

‘’ Ni ukombozi kwetu Watanzania kupata mabehewa kama haya kwa sababu yaliyokuwepo hayana hali nzuri  hivyo itatusaidia sisi kuachana na mabasi,” amesema.

Desemba 6, mwaka huu, jumla ya mabehewa mapya 22  yalikamilisha taratibu za kufanya majaribio kutoka Dare s Salaam - Morogoro na kurudi na LATRA kuridhia kuanza kubeba abiria nchini.

Abiria wakipanda treni ya kwenda Kigoma, katika kituo cha Kamata, Dar es Salaam, ambapo  wamesafiri kwa kutumia mabehewa mapya ya Shirika la Reli (TRC), yaliyowasili hivi karibuni.

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, akimkabidhi dereva wa Treni, Line clear kuanza safari ya kutoka Dar es Salaam had Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TRC, Jamila Mbarouk. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akipeperusha bendera kumruhusu dereva  wa Treni, kuanza safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TRC, Jamila Mbarouk.Abiria abiria wakipanda Treni ya kuelekea Mkoani Kigoma katika kituo cha Kamata Dar es Salaam, jana ambapo kwa mara ya kwanza abiria hao wamesafiri kwa kutumia mabehewa mapya yaliyowasili hivi karibuniAbiria wakipanda Treni ya kuelekea Mkoani Kigoma katika kituo cha Kamata Dar es Salaam, jana ambapo kwa mara ya kwanza abiria hao wamesafiri kwa kutumia mabehewa mapya yaliyowasili hivi karibuni.

Abiria akipitisha mzigo dirishani Baadhi ya abiria wakiwa ndani ya treni hiyo wakipanga mizigo yao