MGODI WA DHAHABU WA BARRICK NORTH MARA, WAKIFURAHIA FAMILY DAY 2022.

Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wakifurahia mchezo wa kubembea wakati wa Family Day ya Mgodi wa Barrick North Mara iliyofanyika mwishoni mwa wiki mgodini hapo.

Watoto wa Wafanyakazi wakishindana kujibu maswali na kupewa zawadi wakati wa Family Day ya Mgodi wa Barrick North Mara iliyofanyika mwishoni mwa wiki mgodini hapo.


Mbunge wa Tarime Vijijini Mh.Mwita Waitara (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu kifaa cha uokozi kutoka kwa mfanyakazi wa Mgodi huo wakati wa maonyesho yaliyofanyika siku hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi, Apolinary Lyambiko.


Washiriki wa bonanza la family Day ya mgodi wa Barrick North Mara wakishiriki mchezo wa kuvuta kamba.

Washiriki wa bonanza la family Day ya mgodi wa Barrick North Mara wakishiriki mchezo wa kukimbia na magunia


 Mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara mwishoni mwa wiki uliandaa tukio la family Day 2022 ambalo lilikutanisha maelfu ya wanafamilia wa wafanyakazi wa Mgodi huo ,viongozi wa Serikali na vijiji vinavyozunguka mgodi, na wakazi wa eneo hilo ambapo waliweza kuungana na kufurahi pamoja kuadhimisha siku hiyo