KATIBU MKUU WA CCM CHONGOLO AONGOZA MKUTANO WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki wanaounda Kamati ya Usimamizi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), Kibaha kwa Mfipa, mkoani Pwani. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha SWAPO, Sophia Shaningwa na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Profesa Marcelina Chijoriga.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Anamringi Macha (kulia) na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, wakishiriki katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki wanaounda Kamati ya Usimamizi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) kilichopo Kibaha kwa Mfipa.

 

NA MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel  Chongolo, ameongoza Mkutano wa kwanza wa  kawaida wa kamati ya uongozi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, mkoani Pwani,

Akitoa taarifa ya mkutano huo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, amesema mkutano huo unajumuisha makatibu wakuu na wawakirishi wa vyama sita Rafiki vya ukombozi kusini mwa Afrika.

 Sophia amevitaja Vyama hivyo ni CCM, FRELIMO (Msumbiji), ZANU-PF (Zimbambwe),  MPLA (Angola), SWAPO (Namibia) na ANC (Afrika kusini).

 Aidha amesema kuwa lengo la mkutano huo ni makatibu wakuu na viongozi wengine na kukagua miundombinu ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere na kupitia na Kujadili taarifa mbalimbali kuhusu uendeshaji wa chuo hiki.

 Pamoja na hayo Sophia, ameeleza malengo ya kuanzishwa kwa shule hiyo ya uongozi ni kuandaa na kufundisha uongozi na uzalendo kwa Makada na wananchi ili kuendelea kujikomboa kiuchumi, kisiasa, kijamii na kifikra, baada ya Ukombozi uliyofanyika wa kuondoa utawala wa kikoloni na kupata uhuru kamili.

Amesema mkutano umeanza Januari 17, 2023 na utamalizika Januari, 19, mwaka huu.