UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) KIPANDE CHA TABORA - ISAKA, KUMEKUCHA, MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango (kulia) na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, wakifurahia baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Tabora hadi Isaka, Shinyanga, yenye urefu wa Kilomita 165, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Isaka Mkoa wa Shinyanga..


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango (kulia) na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, wakiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Tabora Isaka, mkoani Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Tabora Isaka, mkoani  Shinyanga.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, wakati reli ya mfano  inayotarajiwa kujengwa Tabora Isaka, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Isaka, mkoani Shinyanga.