IGP WAMBURA ATOA MAELEKEZO KWA WAKUU WA USALAMA BARABARA, WAKAGUZI WA MAGARI NA WATAHINI WA MADEREVA






 

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura, amefanya  kikao na wakuu wa Polisi wa Usalama barabarani wa Mikoa yote Tanzania, wakaguzi wa magari na watahini wa madereva, katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimelenga kuwakumbusha mambo ya kuzingatia katika utendaji kazi, usimamizi, ufuatiliaji na kuona namna bora ya kuondokana na ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva.

Hii ni sambamba na kutoa mafunzo  kwa wakaguzi wa magari na watahini wa madereva wapya ambao watapewa  mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu.

Akizungumza na waandishi waandishi wa habari, IGP Wambura, amesema jeshi hilo limefanya uchunguzi na kuona umuhimu wa kurekebisha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva ili kudhibiti ajali za barabarani.