MATIBABU YA MOYO NA FIGO KUTOLEWA BURE DAR TAREHE 27 NA 28 MWEZI HUU






 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, OMary Kumbilamoto, amewataka wananchi kujitokeza katika kambi maalumu  ya Moyo na Figo itakayofanyika  Februaru  27 na 28 mwaka huu ambapo vipimo na matibabu  itafanyika bure.

Kambi hiyo inafanyika kituo cha  DSB Poly Clinic   kilichopo Upanga, Mkabala na Msikiti wa Tambaza, Barabara ya Umoja wa Mataifa.

Kambi hiyo imeandaliwa  na kituo hicho kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo mbali na Moyo na Figo, kutakuwa na madaktari mbalimbali wa magonjwa ya binadamu hususan lishe na  watoto na huduma zote zitakuwa ni bure.

UFIKA  panda magari ya kwenda Muhimbili, Barabara ya  Umoja wa Mataifa, Uliza Msikiti wa Tambaza, mkabala na msikiti huo utaona bango la DSB Poly Clinic.