DC HALIMA AMEZITAKA TAASISI KUTENGA FEDHA ZA KUPANDA MITI BAGAMOYO

 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende, wakipanda mti katika Shule ya Misingi Shukuru Kawambwa, Kata ya Kilomo, mkoani Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende, wakimwagilia maji mti, baada ya kuupanda katika Shule ya Misingi Shukuru Kawambwa, Kata ya Kilomo, mkoani Pwani. Kulia ni Mbunge wa Bagamoyo, Mwalamu Mkenge.

 

NA MWANDISHI WETU 

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash, ametoa rai kwa taasisi mbalimbali za serikali na Halmashauri ya Bagamoyo kutenga fedha za upandaji miti.

Halima ametoa rai hiyo, mwishoni mwa wiki, wakati wa hafla ya kupanda miti 1,000, iliyotolewa na benki ya standard Chartered katika Shule ya Msingi Shukuru Kawambwa, Kata ya Kilomo, mkoani Pwani. 

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kuhakikisha ya kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji, hivyo mkurugenzi na timu yake miti yote inapandwa.

Pia Halima amewataka wananchi kwa kila kaya kupanda miti mitano na kila taasisi iliyopo katika halmashauri hiyo na Chalinze wapande miti 30 katika maeneo yao.

Amesema kitendo kilichofanywa na benki hiyo cha kupanda miti kitawafanya watoto waanze kupanda miti wakiwa wadogo na kuwa mabalozi wazuri wa kutunza mazingira.

"Kitendo tunachokifanya cha kuoanda miti itatusaidia kutunza mazingira yetu, pia tuanafundisha wanafunzi wakupanda miti na kutunza mazingira hata wakiwa majumbani mwao", amesema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende, amesema amechukua hatua hiyo ya kupanda miti ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na muelekeo wa muelekeo wa dunia.

Kasekende amesema kuotesha miti mbali na kupata chakula, pia kunasaidia kuondoa hewa chafu na kupata hewa safi ya oksjeni.

Amesema benki hiyo inalichukulia suala la mabadiliko ya hali ya hewa kama moja ya changamoto kubwa zaidi ya mazingira inayokabili ulimwengu wa sasa, kwa kuzingatia athari zake zilizoenea na zilizothibitishwa kwa kuharibu mazingira, afya za binadamu na uwezekano wa kuathiri ukuaji wa uchumi.

Kasekende amesema wamelenga kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuunga mkono mabadiliko ya jumla ya kufika sifuri kwa hewa chafu, kukabiliana na athari za hali ya hewa.

"Upandaji miti unapunguza uharibifu wa mazingira, kwa zaidi ya miaka 10, tumepanda miti katika shule mbalimbali za msingi, tunapanda miti 1,000 katika Shule hii Shukuru Kawambwa, kama sehemu ya dhamira yetu ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi", amesema.

Kwa upande wa  Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Fatuma Kisimbo, amesema sehemu kubwa ya shule yao haina miti, miti inayopandwa na benki hiyo itasaidia kuweka vivuli kuwasaidia wanafunzi kupumzika wanapotoka madarasani.

Amesema wamejiandaa kuitunza miti hiyo na kwamba kila mwanafunzi amepewa miti mitano ya kuihudumia, pia miti hiyo itasaidiakupunguza hewa chafu na kuongeza kupatikanaji wa hewa ya oksjeni shuleni hapo.

"Wakati wa jua kali wanafunzi wetu wanapata taabu kukaa katika sehemu za kupumzikia, pia benki ya Standar Chartered imetumeletea miti ya matunda ambayo baada ya kukua tutapata matunda na kupelekea kuimalika kwa afya za wanafunzi wetu", amesema. 

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash, akizungumza wakati wa upandaji miti 1,000, iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered, mkoani Pwani.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende, akizungumza wakati hafla ya kupanda 1,000, iliyotolewa na benki hiyo katika Shule ya Msingi Shukuru Kawambwa, wilayani Bagamoyo, Pwani. 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shukuru Kawambwa, akizungumza katika hafla hiyo.

Wananchi Bagamoyo na Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered, wakifuatilia hafla ya upandaji miti katika shule hiyo.