KAMPUNI YA BARRICK YAENDELEZA REKODI YA USHINDI TUZO ZA WIKI YA OSHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako,  akikabidhi tuzo ya OSHA  mshindi wa jumla  wa maonyesho ya OSHA  Mkufunzi wa Usalama mahali pa kazi wa Barrick  Bulyanhulu,  Azaely Kitenge, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi  wa washindi, mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA),  Dkt. Adelhelm Meru.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick, wakifurahia tuzo ambazo migodi yake imenyakua wakati wa maonyesho ya OSHA, wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki.


 

MOROGORO

Barrick Tanzania imeshinda tuzo sita katika hafla ya utoaji wa tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya 2023 iliyofanyika mjini Morogoro kwa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kushinda tuzo kubwa kubwa ya mshindi wa juu wa Jumla katika Tuzo ya  Afya na Usalama (OHS) za mwaka 2023.

Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu pia ilinyakua tuzo ya uandaaji Ripoti Bora ya Tathmini ya Hatari katika  uchimbaji madini na mshindi Bora wa tuzo ya Usalama na afya (OHS) katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Barrick North Mara ilishinda tuzo za juu katika: Kujali Zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum na  kutekeleza sera Bora ya Usalama mahali pa kazi (OHS). Pia ilikuwa mshindi wa pili kwa washindi wa jumla wa sekta ya Madini.

Mwaka huu Mgodi wa Buzwagi pia ulishiriki maonesho hayo na kunyakua  tuzo ya utekelezaji Mpango Kazi Bora wa Usalama na Afya mahali pa kazi.

Maonyesho ya OSHA mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako, alikuwa mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwaka huu.

Barrick Tanzania imeshinda tuzo za 2023 kutokana na mafanikio ya 2022 ya kampuni ambapo ilishinda tuzo za jumla ikiwemo tuzo ya mshiriki wa maonyesho na tuzo ya kuzingatia kanuni za usalama

Usalama ni sehemu muhimu ya DNA ya Barrick. Kampuni ina mpango maalum kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake na wakandarasi, kuhakikisha kwamba kila mtu anarudi nyumbani akiwa na afya njema na salama. Juu ya yote hayo katika Barrick kila mtu amejitolea kufanya analoweza kuhakikisha hakuna matukuo ya ajali katika sehemu yake anapofanyia kazi.