BALOZI WA MAREKANI NCHINI AJITAMBULISHA IKULU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,  amesisitiza kuwa Serikali inaunga mkono uwekezaji katika maeneo ya uchumi wa Buluu ikiwemo usafirishaji wa baharini, mafuta na gesi, na bandari. 

Rais Dk. Mwinyi, ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipotembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Anthony Battle kujitambulisha.

Dk. Mwinyi amesema kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumetokana na makubaliano yaliyofanyika baada ya uchaguzi ili kutafuta njia za kutatua tofauti zilizopo ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuendesha na kudumisha amani na utulivu nchini. 

Naye, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Anthony Battle ameridhishwa na utendaji wa Rais Dk. Mwinyi kwa utayari wake katika sekta ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Marekani imelenga kuwekeza zaidi nchini na kutoa fursa za ajira.