JUMUIYA YA WAZAZI CCM KATA YA ILALA, WANACHAMA WA CCM NA WANANCHI WACHANGIA DAMU

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ilala, Sabry Sharif, akichangia damu katika kambi maalumu iliyoandaliwa na jumuiya hiyo wakati wa Fainali za Wazazi Cup, Uwanja wa Garden Ilala. Kambi hiyo maalumu ililenga wananchi  wote na wanachama wa CCM kuchangia damu kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama, ikiwa ni hatua ya kuhitimisha michuano hiyo ya Wazazi Cup.