MAKALLA ATANGAZA KUANZA KWA AWAMU YA PILI YA PENDEZESHA DSM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, ametangaza kuanza kwa awamu ya pili ya kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM, baada ya awamu ya kwanza ya kampeni hiyo iliyodumu kwa mwaka Mmoja na miezi mitano kuwa na mafanikio Makubwa.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha tathimini awamu ya kwanza na kuweka mikakati ya awamu ya pili, Makalla amewaelekeza watendaji kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Mitaa kusimamia ufanyaji Usafi.

Amesema miongoni mwa mambo yayopaswa kuwekewa mkazo zaidi ni udhibiti wa ufanyaji biashara holela, usafishaji mazingira, upendezeshaji na upandaji miti kwenye bustani.

Aidha Makalla ameelekeza kila Halmashauri kushirikiana na wadau ambao wapo tayari kupendezesha Jiji, huku akielekeza Taasisi za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), TARURA na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA)  kufanya kazi kwa ushirikiano.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kufanya Dar es salaam izidi kushika nafasi za juu kwa usafi Afrika, jambo litakalosaidia kudhibiti pia mlipuko wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na hata kudhibiti maambukizi ya malaria.

Pia Makalla amsisitiza wananchi kufanya usafi killa Jumamos ya mwisho wa mwezi,  huku akiwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye Maeneo waliyopangwa.