RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA MSAADA WA MAENDELEO INAYOFADHILIWA NA EU

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa waka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. Mikataba hiyo imetiwa Saini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Nchini Mhe. Manfredo Fantl katika Ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma 04 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kwenye Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya Msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni  455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma tarehe 04 Julai, 2023.