RC CHALAMILA AMWAPISHA DC TEMEKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Albert Chalamila, amemwapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Mobhare  Matinyi na kutaka viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Manispa ya Temeke kumpa ushirikiano.

Matinyi  ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahamis Munkunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Hafla ya uapisho huo ilifanyika, Dar es Salaam,  katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkoa  na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekretarieti na wilaya za mkoa huo wakiongozwa na katibu Tawala wa Mkoa, Rehema Madenge.

Chalamila amemtakia majukumu mema  Matinyi katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Temeke huku akisisitiza vingozi wa  halmashauri hiyo kumpa ushirikiano.