Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mapata Tanzania (TRA), imeboresha mifumo yake ya kutoa huduma kwa njia mtandao (Taxpayer Portal), ili kuwarahishia wananchi wengi kupata huduma mbalimbali.
Akizungumza katika Maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara, yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Ofisa Msimamizi wa Kodi za Ndani wa TRA, Hamis Sanze, amesema huduma zilizoboresha ni usajili wa kupata namba ya mlipakodi (TIN NUMBER) kwa kampuni na watu binafsi, kutuma mizigo nje na ndani ya nchi.
Sanze amesema huduma zingine zilizoboreshwa na TRA ni kuingiza mizigo bandarini, viwanja vy ndege na mipakani, kurekebisha stakabadhi zilizokosewa na ritani za watu wasio wakazi.
Pia Sanze amesema TRA imeboresha huduma katika kufanya malipo ya tathimini ya kodi, kuomba usajili kwa njia ya mtandao na kutambua uhalali wa leseni pamoja na usajili wa vyombo vya usafiri ikiwemo kadi zilizopotea au kutaka nakala kwa waliouziana gari au pikipiki na kubadilisha umiliki.