RC SERUKAMBA-WANANCHI SINGIDA PANDENI MITI KUTUNZA MAZINGIRA


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoka kukagua mradi wa ICU katika hospitali ya wilaya ya Iramba mjini Kiomboi, alipofanya ziara wilayani humo kujionea vifaa tiba vya kisasa vilivyonunuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba. (Picha na Hemedi Munga)




Na HEMEDI MUNGA

Wananchi wilayani Iramba Mkoani Singida, wametakiwa kuwa na  tabia ya kupanda miti katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanaendelea kuvutia muda wote.

Akizungumza na baadhi ya viongozi punde baada ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo, Mkuu  wa Mkoa huo, Peter Serukamba amewaagiza viongozi kuhakikisha miti mingi inapandwa kuzunguka miradi hiyo kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanaendelea kubakia vema.

Serukamba ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi anuai inayotekelezwa wilayani Iramba mkoani hapa.

"Tujitahidi katika kila mradi wetu kuwe na miti na kujiepusha na ukataji wa miti," amesisitiza.

Aidha, amehimiza usafi ufanyike kikamilifu ambao utaacha maeneo mbalimbali kuwa katika hali yakuendelea kuvutia muda wote.

Mkuu huyo ametembelea mradi wa shule ya msingi Ishanga, Ofisi ya masijala ya Ardhi Masagi, vifaa tiba vya kisasa hospitali ya wilaya Old Kiomboi  na mradi wa maji Makunda.