WANANCHI IRAMBA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS DK. SAMIA

.Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Mkoa wa  Singida, Warda Obathany, akisoma risala ya utii kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023,  katika kiwanja cha CCM Lulumba mjini Kiomboi.  (Picha na Hemedi Munga)


IRAMBA - SINGIDA 

Na HEMEDI MUNGA 

Wananchi wilayani Iramba Mkoa wa  Singida, wamemuhakikishia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wataendelea kumuunga mkono na kuahidi kumpa kura za kishindo ifikapo 2025 katika uchaguzi mkuu.


Akisoma Risala ya Utii kwa Rais huyo, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Warda Obathany amesema kuwa wanaungana na Rais Samia kwa nguvu zote katika kuhamasisha wananchi kuitekeleza kivitendo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu.


"Tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa," amenukuu.


Aidha, Warda amempongeza Rais kwa jitihada anazozifanya kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali ikiwemo kupambana na rushwa, ufisadi, kusimamia watu, uwajibikaji, kuinua ubora wa elimu, kutoa huduma za afya na kurejesha maadili nchini.